Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameipongeza Rwanda kwa kurudisha mashindano ya Formula 1 barani Afrika.
Kupitia X, Ramaphosa ameandika" Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Afrika Kusini, ninatoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais Serikali na wananchi wa Rwanda kwa kupata mkataba wa miaka 10 wa kuandaa mashindano ya Formula 1 African Grand Prix."
"Afrika Kusini inashiriki fahari ambayo Rwanda inayo wakati ikijiandaa kupeperusha bendera ya ushindi kwa niaba ya bara letu, kwa kuandaa mashindano haya yenye hadhi kubwa duniani katika uwanja wa mashindano uliopangwa kujengwa Bugesera kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2030. Mkataba huu ni utambuzi wa uwezo wa taifa la Rwanda na wa bara letu kwa ujumla." Ramaphosa ameongeza
Rais Ramaphosa amesisitiza nchi yake itatoa msaada ikewezekana. " Kama nchi iliyoandaa mashindano ya kwanza ya Grand Prix kufanyika katika ardhi ya Afrika mwaka 1993, na kuandaa matukio mengine makubwa ya kimataifa, Afrika Kusini itafurahi kutoa msaada wowote tutakaoombwa kushiriki."
Ni mara ya pili Formula 1 kuandaliwa barani Afrika.


