Bwiza

Mshtuko Burundi: Kijana Mseremala Afariki Baada ya Kupigwa na Hakimu na Polisi Wawili

Habari
Fred Karege
By Fred Karege
Kuwa Kabiri, 22 Nyakanga 2025 saa 05:40
Iminota 1 yo gusoma3 Abasomye
Mshtuko Burundi: Kijana Mseremala Afariki Baada ya Kupigwa na Hakimu na Polisi Wawili

Kijana mmoja mseremala alifariki dunia siku mbili baada ya kupigwa vibaya na polisi wawili pamoja na hakimu. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea tarehe 16 Julai katika komini ya Tangara, mkoa wa Butanyerera, kaskazini mwa Burundi. Watumishi hao watatu wa serikali walikamatwa na kuwekwa kizuizini Ngozi.

Mashahidi kadhaa wamesema tukio hilo lilitokea katika mgahawa mmoja ambapo Donatien Nduwimana alikuwa akifanya kazi ya kutoa huduma ya chakula.

Inadaiwa kuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo ya Tangara hakuridhishwa na huduma aliyopokea na namna sahani aliyoletewa ilivyokuwa, ndipo akaanza kumpiga kijana huyo kwa ukatili mkubwa.

Kwamamaza (728x90)

Umwanya w'Iyamamaza ry'Ubucuruzi - BWIZA ADS

Kwamamaza hano: isaackamis@gmail.com | +250 788 000 000

Baadaye alimpigia simu polisi wawili ambao badala ya kuingilia kati kuzuia vurugu, walimsaidia kumpiga mhudumu huyo wa mgahawa.

Donatien Nduwimana alikimbizwa hospitali ya Ngozi ambapo alifariki tarehe 18 Julai kutokana na majeraha aliyopata, kwa mujibu wa SOS Medias Burundi.

Mwendesha mashtaka aliamuru kukamatwa kwa watatu hao wanaoshukiwa kuhusika. Wanazuiliwa katika gereza la Ngozi huku uchunguzi ukiendelea.

Fred Karege

Inkuru yanditswe na: Fred Karege

Umunyamakuru wa BWIZA.COM wanditse inkuru 2,508.